Al-Qiyaas na Nusoos (matini):
Al-Qiyaas and the Nusoos (texts):
Inawezekana kuwepo mgongano au upingamizi kati ya Hukmu inayotokana na Nass (maandishi ya Qur'ani au Sunnah) na Hukmu ya Far'u (tawi) inayopatikana kwa Al-Qiyaas.
It is possible for there to be a conflict or contradiction between the Hukm that is taken from the Nass (text) and the Hukm of the Far’u (branch) that is deduced by Al-Qiyaas.
Inawezekana kufupisha maoni ya Fuqahaa' kuhusiana na Mas'alah (suala) hili katika makundi matatu:
It is possible to sum up the opinions of the Fuqahaa’ in relation to this Mas’alah (issue) into three categories:
1) Ikiwa hukmu inayotokana na maandiko inapingana na hukmu ya tawi lililopatikana kwa Qiyaas, basi inachukuliwa hukmu inayofahamika kutoka kwenye maandiko, kwa sababu hakuna kabisa Qiyaas pale maandiko yanapokuwepo. Hili linatumika iwe maandiko ni Qat'iy au Zhanniy, na iwe maana (Dalaalah) ya maandiko ni Qat'iy au Zhanniy. 2) Hukmu ya tawi lililochukuliwa kwa Qiyaas inaweza kupingana na hukmu nyingine inayotokana na maandiko kwa Dalaalah Zhanniy (maana isiyo dhahiri), lakini haiwezi kupingana na ile Qat'iy.