Ushahidi wa hilo ni kama ifuatavyo:
The evidence for that is as follows:
Haijuzu kwa ijtihadi kuhusishwa kwa Mjumbe wa Allah ﷺ.
It Is Not Permitted For Ijtihaad To Be Attributed To The Messenger Of Allah (saw)
1 – Ushahidi wa Akili (Dalili ya kiakili):
1 – Ad-Daleel Al-‘Aqliy (Rational or intellectual evidence):
Dhana ya Ijtihaad inapingana na 'Ismah (kutokukosea) ya Mtume ﷺ kwa sababu haijuzu kwamba kosa litokee kuhusu ujumbe (Ar-Risaalah) na ufikishaji (At-Tableegh). Kwa hiyo Mtume ﷺ hakosei kuhusu ujumbe na ufikishaji, na ni kwa sababu hiyo tumeamrishwa kumfuata Mtume ﷺ katika yale anayotufikishia kutoka kwa Mola wake. Ijtihaad kwa upande mwingine inaweza kukosea, na si jambo linalowezekana kiakili kwa Allah kutuamrisha kufuata kosa.
The concept of Ijtihaad is contradictory to the ‘Ismah (infallibility) of the Messenger (saw) because it is not permitted for error to occur in respect to the message (Ar-Risaalah) and conveyance (At-Tableegh). The Messenger of Allah (saw) is therefore infallible from an error in respect to the message and the conveyance and because we have been commanded to follow the Messenger (saw) in respect to that which he conveys to us from his Rabb. That is whilst Ijtihaad is open to error and it is not intellectually conceivable for Allah to command us to follow the error.
2 – Ushahidi wa Kishari'a (Ad-Daleel Ash-Shar'iy):
2 – Ad-Daleel Ash-Shar’iy:
Mwenyezi Mungu Ta'ala amefahamisha katika Qur'ani Tukufu kwamba Mjumbe ﷺ huonya kwa Wahyi tu, na husema au kutamka kwa Wahyi tu (ufunuo wa kimungu). Mwenyezi Mungu (SWT) amesema:
Allah Ta’Aalaa has informed in the Qur’aan Al-Kareem that the Messenger (saw) only warns by the Wahi and only speaks or utters from the Wahi (divinely inspired revelation). Allah (swt) said:
Sema: “Ninawaonya kwa wahyi tu” (Al-Anbiyaa’ 45).
Say: “I warn you only by the revelation” (Al-Anbiyaa’ 45).
Na Yeye Ta'ālā alisema:
And He Ta’Aalaa said:
Wala hasemi kwa matamanio yake.Hayo si chochote isipokuwa ni wahyi unaofunuliwa (An-Najm 4)
Nor does he speak of (his own) desire. It is only a revelation that is inspired (An-Najm 4)
Hali hii ilithibitishwa na matukio halisi. Hiyo ni kwa sababu tatizo lilipojitokeza au tukio lilipotokea, alichelewesha kujibu swali au kutoa hukumu juu ya uhalisia huo, mpaka Wahyi ulipomteremkia ﷺ; baadhi yake lilimjia upesi, na mengine yalimjia baada ya siku kadhaa. Kwa hiyo hakufanya Ijtihaad ili kujibu, bali alisubiri jibu au Hukm kutoka kwenye Wahyi. Allah (SWT) amesema:
The realities proved this. That is because when an issue arose or an incident occurred, he delayed answering the question or passing judgment upon the reality, until the Wahi had been revealed upon him, some of which came to him quickly whilst some of it came after days. And so he did not undertake Ijtihaad in order to respond but rather he waited for the answer or the Hukm from the Wahi. Allah (swt) said:
Mimi situfuati chochote isipokuwa kile ninachofunuliwa kwa wahyi. (Al-An'aam 50)
I but follow what is revealed to me by inspiration (Al-An’aam 50).