Jinsi Qur'ani ilivyoteremshwa
How the Qur’an was revealed
Qur'ani iliteremshwa kwa Nabii Muhammad ﷺ kwa vipande (sehemu) kwa muda wa miaka 23. Haikushuka kwa mpangilio maalum; wakati mwingine ilikuja mfululizo, na wakati mwingine ilichelewa au kulikuwa na mapengo marefu kati ya wahyi mmoja na mwingine. Wa kwanza kuteremshwa ulikuwa kutoka Suratul 'Alaq, na huo ulikuwa ni Kauli Yake Ta'ala:
The Qur’aan was revealed upon the Nabi Muhammad (saw) in instalments (in parts) over a period of 23 years. It did not descend upon a regular pattern; sometimes it would come consecutively whilst at other times it would be delayed or there would be long gaps between the revelations. The first to be revealed was from Soorah Al- ‘Alaq and this was His Qawl Ta’Aalaa:
Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba. Aliumba mwanadamu kutokana na pande la damu. Soma, na Mola wako ndiye Mkarimu zaidi. Aliyefundisha kwa kalamu. Alimfundisha mwanadamu asiyoyajua. (Al-‘Alaq 1-5)
Read in the name of your Lord who created. Created man from a clot. Read and your Lord is the Most Generous. Who taught by the pen. Taught the human that which he did not know (Al-‘Alaq 1-5).
Na ufunuo wa mwisho kabisa ulikuwa ni kauli ya Allah Ta'aalaa:
And the last of the revelation was the speech of Allah Ta’Aalaa:
Na mcheni Siku ambayo mtarejeshwa kwa Allah. Kisha kila nafsi italipwa kwa yale iliyoyachuma, nao hawatadhulumiwa (Al-Baqarah 281).
And fear a Day when you will be returned to Allah. Then every soul will be compensated for what it earned, and they will not be treated unjustly (Al-Baqarah 281).
Qur'ani ilianza kuteremshwa kwa Mjumbe wa Allah ﷺ alipokuwa katika pango la Hiraa', karibu na Makka, ambapo alikuwa akienda kwa ajili ya kujitenga na kutafakari kabla hajakabidhiwa jukumu la kubeba ujumbe na Unabii.
The Qur’aan began to be revealed upon the Messenger of Allah (saw) when he was in the cave of Hiraa’, close to Makkah, where he would go for solitude and to contemplate before he was tasked with the carrying of the message and the Prophethood.