Aqsaam (Makundi) ya Waajib kwa Kuzingatia Nani Ni Mukallaf (yaani, Nani Amepewa Jukumu la Kutekeleza Wajibu)
The Aqsaam (categories) Of The Waajib In Relation To The Consideration Of Who Is Mukallaf (i.e. Who Has Been Charged To Undertake The Obligation)
1 – Waajib ‘Ainiy au “Fard ‘Ain” Hiki ndicho ambacho Ash-Shaari' ameagiza kifanywe na kila Mukallaf, na si jambo linalotosha kwa baadhi ya watu kukifanya huku wengine wakiacha kukifanya. Mifano ya hili ni Swalah, Saumu, kutimiza ahadi na mikataba, na Zakaah. Basi mwenye kuacha kitendo hicho anakuwa na dhambi, na mtu mwingine kukifanya kitendo hicho hakumwondolei dhambi hiyo.
1 – Waajib ‘Ainiy or “Fard ‘Ain” This is what the Shaari’ has requested to be done from every Mukallaf and it is not sufficient for some to do it whilst others do not. Examples of this include the Salaah, the Sawm, being faithful to contracts and the Zakaah. The one who leaves the action is therefore sinful and another person’s undertaking of it does not remove that sin from him.
2 – Waajib ‘Alaa Al-Kifaayah:
2 – Waajib ‘Alaa Al-Kifaayah:
Hii ndiyo ambayo Shaari' (Mwekaji wa Sheria) ameitaka itekelezwe na kundi (jamaa'ah) la Mukallafeen (wala si wote). Pindi baadhi yao wanapoitekeleza, basi wajibu huo unawaondokea waliobaki na hakuna dhambi juu yao. Bali wote watakuwa wenye dhambi ikiwa wajibu wa kifaayah (kutosheleza) hautimizwi. Mifano ya hili ni Al-Jihaad, uamuzi wa mahakama, kueneza Da'wah ya Kiislamu ili kuanzisha Dola ya Kiislamu, kuanzisha viwanda na sayansi au nyanja za maarifa ambazo Ummah unazihitaji, kuandaa nguvu inayohitajika ili kumtia adui hofu, na kumswalia maiti na kumzika.
This is what the Shaari’ (Legislator) has requested to be undertaken by a Jamaa’ah (collective) of the Mukallafeen (and not all of them). If or when some have undertaken it, then it (the obligation) falls from the rest and there is no sin upon them. Rather, all are sinful if the Waajib upon the Kifaayah (sufficiency) is not met. Examples of this include Al-Jihaad, judiciary, carrying the Islamic Da’wah to establish the Islamic State, generating industries and sciences or areas of knowledge that the Ummah is in need of, preparing the necessary force to strike fear into the enemy and praying over the dead and burying them.