Q 13: Uislamu ni nini?
Q 13: What is Islam?
Islamu maana yake ni kujisalimisha kikamilifu na kunyenyekea kabisa kwa Allah; na kushuhudia Tauhidi kamili na kujiepusha na ushirikina na kutomtii Yeye.
A--- Islam means perfect submission and subjection to Allah; and testifying complete Monotheism and freedom from polytheism and disobedience to Him.
Allah, Aliye Juu, anasema: {Na ni nani aliye bora zaidi katika dini kuliko yule anayejisalimisha kwa Allah}. (An-Nisaa, 125)
Allah, Most High says: {And who can be better in religion than one who submits his fate (himself) to Allah}. (AnNisa', 125)
Anasema: {Na atakayejisalimisha uso wake kwa Mwenyezi Mungu, naye ni mwenye kuhsini, basi amekamata kishikio kilicho imara zaidi}. (Luqman, 22)
He says: {And whosoever submits his face (himself) to Allah, while he is a Muhsin, then he has grasped the most trustworthy handhold}. (Luqman, 22)
Anasema: {Na Mungu wenu ni Mungu Mmoja, basi jisalimisheni Kwake peke yake (katika Uislamu). Na (Ee Muhammad) wabashirie wanyenyekevu}. (Al-Hajj, 34)
He says: {And your Ilah (god) is One Ilah (God -Allah), so you must submit to Him Alone (in Islam). And (O Muhammad) give glad tidings to the Mukhbitun}. (Al-Hajj, 34)
Marejeo: 200 FAQ On Muslims Belief - Shiekh Hafiz Ibn Ahmed Al Hakami
Reference: 200 FAQ On Muslims Belief - Shiekh Hafiz Ibn Ahmed Al Hakami