Q 188: Madhambi yanafutwaje?
Q 188: How are sins expiated?
A--- Allah Mtukufu asema: {Mkiepuka madhambi makubwa mliyokatazwa kuyafanya, Tutakufutieni madhambi yenu madogo, na Tutakuingizeni mahali pa heshima (yaani Peponi)}. (An-Nisaa', 31)
A--- Allah the Almighty says: {If you avoid the great sins which you are forbidden to do, We shall expiate from you your (small) sins, and admit you to a Noble Entrance (i.e. Paradise)}. (An-Nisa', 31)
Allah Mtukufu Mwenye Enzi anasema: {Hakika mema huyafuta maovu (yaani madhambi madogo)}. (Hud, 114)
Allah the Almighty says: {Verily, the good deeds remove the evil deeds (i.e. small sins)}. (Hud, 114)
Hivyo basi, Mwenyezi Mungu Mtukufu ametujulisha kwamba dhambi zinafutwa kwa kujiepusha na kutenda dhambi kubwa na kwa kufanya matendo mema. Aidha, Hadithi inasema: "Na fanya tendo jema baada ya dhambi ili liifute." (Ahmad, At-Tirmidhi, Al-Hakim)
Thus, Almighty Allah informed us that sins are being expiated by means of avoiding committing the Major sins and performing good deeds. In addition, the Hadith says: "And do a good deed after a sinful one to remove it.” (Ahmed, At-Tirmidhi, AI-Hakim)
Aidha, Hadithi sahihi zinaeleza kwamba matendo haya ya utii pamoja na mengine yanafuta dhambi na makosa: matendo hayo ni kama yafuatayo: kutawadha vizuri kabisa, kutembea kwenda misikitini kwa ajili ya Sala, kusali Sala tano za faradhi, kuhudhuria Sala ya Ijumaa, kufunga mwezi wa Ramadhani, kusimama kwa Sala usiku wake na hasa Usiku wa Lailatul-Qadr, na kufunga siku ya 'Ashuraa. Hata hivyo, Hadithi nyingi kati ya hizi zinasharti kwamba mtu aepuke kutenda dhambi kubwa.
In addition, the authentic Hadiths state that the following deeds of obedience along with others expiate sins and misdeeds: these acts are as follows: performing perfect ablution, walking to the mosques for prayer, performing the five compulsory prayers, Friday Prayers attending, fasting Ramadan, standing in prayer through its nights and the Night of Might in particular, and fasting during the day of 'Ashuraa’. However, most of these Hadiths stipulate that one should avoid committing the Major sins.
Kwa hiyo, kujiepusha na madhambi makubwa ni sharti la kufutiwa madhambi madogo kwa kutenda mema.
Thus, avoiding the Major sins is a precondition for expiating the Minor sins through performing good deeds.
Marejeo: 200 FAQ On Muslims Belief - Shiekh Hafiz Ibn Ahmed Al Hakami
Reference: 200 FAQ On Muslims Belief - Shiekh Hafiz Ibn Ahmed Al Hakami