Q 65: Ni dalili gani ya kimaandiko kutoka katika Qur'ani Tukufu kwamba Allah yuko juu kimahali?
Q 65: What is the textual proof from the Glorious Qur'an that Allah is High in Place?
A--- Allah Mtukufu Mwenye Enzi anasema: {Mwingi wa Rehema (Allah) alilingana juu ya (Istawa) Kiti cha Enzi (kwa namna inayolingana na Utukufu Wake)}. (Ta-Ha, 5)
A--- Almighty Allah says: {The Most Gracious (Allah) rose over (Istawa) the (Mighty) Throne (in a manner that suits His Majesty)}. (Ta-Ha, 5)
Allah anasema: {Je, mnajiona mko salama kwamba Yeye, Aliye juu ya mbingu (Allah), hatakufanya ardhi izame pamoja nanyi, kisha ikatetemeka? Au mnajiona mko salama kwamba Yeye, Aliye juu ya mbingu (Allah), hatawatumia upepo mkali wa kimbunga?}
Allah says: {Do you feel secure that He, Who is over the heaven (Allah), will not cause the earth to sink with you, and then it should quake? Or do you feel secure that He, Who is over the heaven (Allah), will not send against you a violent whirlwind?
Basi mtajua jinsi (ilivyokuwa) onyo Langu lilivyo kuwa kali. (Al-Mulk, 16, 17)
Then you shall know how (terrible) has been My Warning}. (AlMulk, 16, 17)
Allah Mtukufu anasema: {Wanamwogopa Mola wao aliye juu yao}. (An-Nahl, 50)
Allah the Almighty says: {They fear their Lord above them}. (AnNahl, 50)
Allah Mtukufu asema: {Kwake hupanda maneno mazuri, na amali njema huinuliwa nayo}. (Fatir, 10)
Allah the Almighty says: {To Him ascend (all) the goodly words, and the righteous deeds exalt it}. (Fatir, 10)
Allah Mtukufu anasema: {Malaika na Ruh [Jibril (Gabriel)] wanapanda kwake katika Siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu hamsini}. (Al-Ma'arij, 4)
Allah the Almighty says: {The angels and the Ruh [Jibril (Gabriel)] ascend to Him in a Day the measure whereof is fifty thousand years}. (Al-Ma' arij, 4)
Allah Mtukufu asema: {Anaendesha na kupanga kila jambo kuanzia mbinguni hadi ardhini}. (As-Sajdah, 5)
Allah the Almighty says: (He manages and regulates (every) affair from the heavens to the earth}. (As-Sajdah, 5)
Allah Mtukufu anasema: {Na (kumbukeni) pale Mwenyezi Mungu alipomwambia: "Ee Isa (Yesu)! Nitakuchukua na kukuinua kwangu}. (Al-Imran, 55)
Allah the Almighty says: {And (remember) when Allah said: "0 'Isa (Jesus)! I will take you and raise you to Myself}. (Al' Imran, 55)
Marejeo: Maswali 200 Kuhusu Imani ya Waislamu - Sheikh Hafiz Ibn Ahmed Al Hakami
Reference: 200 FAQ On Muslims Belief - Shiekh Hafiz Ibn Ahmed Al Hakami