Q 53: Taja mifano fulani ya Majina Mazuri Zaidi ya Allah kutoka katika Qur'ani Tukufu?
Q 53: Cite some examples on the Most Beautiful Names of Allah from the Glorious Qur'an?
A- Allah Subhanahu wa Ta'ala anasema: {Hakika, Allah ni Mtukufu, Mkuu kabisa}. (An-Nisa', 34)
A- Almighty Allah says: {Surely, Allah is Ever Most High Most Great}. (An-Nisa', 34)
Allah anasema: {Hakika Allah ni Mwenye kuwa mpole sana, Mwenye kujua yote kwa undani}. (Al-Ahzab, 34)
Allah says: {Verily, Allah is Ever Most Courteous, Well-Acquainted with all things}. (Al-Ahzab, 34)
Allah anasema: {Hakika Yeye ni Mjuzi wa kila kitu, Mwenye uwezo wa kila kitu}. (Fatir, 44)
Allah says: {Verily, He is All-Knowing, All Omnipotent}. (Fatir, 44)
Allah asema: {Hakika Allah ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona}. (An-Nisaa', 58)
Allah says: {Truly, Allah is Ever All-Hearer, All-Seer}. (An-Nisa',58)
Allah anasema: {Hakika Allah ni Mwenye nguvu zote, Mwenye hekima}. (An-Nisa', 56)
Allah says: (Truly, Allah is Ever Most Powerful, All-Wise}. (AnNisa', 56)
Allah anasema: {Hakika Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu}. (An-Nisaa', 23, 106)
Allah says: {Verily, Allah is Oft-Forgiving, Most Merciful}. (AnNisa', 23, 106)
Hakika Yeye kwao amejaa Upole, Mwenye Rehema sana. (At-Tawbah, 117)
Allah says: {Certainly, He is unto them full of Kindness, Most Merciful}. (At- Taubah, 117)
Allah Mtukufu anasema: {Na Allah ni Mwenye kutosheka (asiye na haja na yeyote) na ni Mwenye kuvumilia sana}. (Al-Baqarah, 263)
Allah the Almighty says: {And Allah is Rich (Free of all needs) and He is Most-forbearing}. (Al-Baqarah, 263)
Allah Mtukufu asema: {Hakika Yeye (Allah) ndiye Mwenye kusifiwa, Mtukufu}. (Hud, 73)
Allah the Almighty says: {Surely, He (Allah) is All-Praiseworthy, All-Glorious}. (Hud, 73)
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Hakika Mola wangu ni Mlinzi juu ya kila kitu}. (Hud, 57)
Allah the Almighty says: {Surely, my Lord is Guardian over ill things}. (Hud, 57)
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Hakika Mola wangu yuko karibu (kwa ujuzi wake wa kila kitu), ni Mwenye kuitikia}. (Hud, 61)
Allah the Almighty says: {Certainly, my Lord is Near (to all by His Knowledge), Responsive}. (Hud, 61)
Allah Mtukufu anasema: {Hakika Allah daima ni Mwangalizi juu yenu}.
Allah the Almighty says: (Surely, Allah is Ever an All-Watcher over you}.
(An-Nisa', 1)
Allah Mtukufu asema: (Na Allah ndiye Mwenye kutosheleza kama Msimamizi wa mambo). (An-Nisa', 81, 132, 171 na Al-Ahzab, 3, 48)
Allah the Almighty says: (And Allah is Ever All-Sufficient as a Disposer of affairs}. (An-Nisa', 81, 132, 171 and Al-Ahzab, 3, 48)
Allah Mtukufu Mwenye Enzi anasema: {Na Allah anatosha kuwa Mwenye kuhesabu}. (An-Nisa', 6 na Al-Ahzab, 39)
Allah the Almighty says: {And Allah is All-Sufficient in taking account}. (An-Nisa', 6 and Al-Ahzab, 39)
Allah Mtukufu anasema: {Na Allah daima ana uwezo juu ya kila kitu, na ni Shahidi juu ya kila kitu}. (An-Nisa', 85)
Allah the Almighty says: {And Allah is Ever All-Able to do (and also an All- Witness to) everything}. (An-Nisa', 85)
Allah Mtukufu amesema: {Hakika Allah ni Shahidi juu ya kila kitu}.
Allah the Almighty says: {Verily! Allah is over all things a Witness}.
(Al-Hajj, 17)
Allah Mtukufu asema: {Hakika Yeye ndiye Anayezunguka kila kitu}. (Fussilat, 54)
Allah the Almighty says: {Verily! He it is Who is surrounding all things}. (Fussilat, 54)
Allah Mtukufu asema: {Allah! Hakuna mungu wa haki isipokuwa Yeye, Aliye Hai milele, Msimamizi wa kila kitu. Usingizi wala usingizi mzito humshiki. Ni Yake yaliyo mbinguni na yaliyo ardhini. Ni nani atakayeweza kuombea mbele Yake isipokuwa kwa idhini Yake? Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kujua chochote katika elimu Yake isipokuwa kile Anachotaka. Kursi Yake imeenea mbingu na ardhi, wala kuvilinda hivyo hakumchoshi. Naye ni Mwenye Kuinuka Juu, Mkuu}.
Allah the Almighty says: {Allah! La ilaha illa Huwa (none has the right to be worshipped but He), the Ever Living, the One Who sustains and protects all that exists. Neither slumber nor sleep overtakes Him. To Him belongs whatever is in the heavens and whatever is on the earth. Who is he that can intercede with Him except with His Permission? He knows what happens to them (His creatures) in this world, and what will happen to them in the Hereafter. And they will never compass anything of His Knowledge except that which Hewills. His Kursi17 extends over the heavens and the earth, and He feels no fatigue in guarding and preserving them. And He is the Most High, the Most Great}.
(Al-Baqarah, 255)
Allah anasema: {Allah! La ilaha illa Huwa (hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Yeye), Aliye Hai milele, Mwenye kusimamia na kulinda kila kilichopo}. (Al-Imraan, 2)
Allah says: {Allah! La ilaha illa Huwa (none has the right to be worshipped but He), the Ever Living, the One Who sustains and protects all that exists}. (Al' Imran, 2)
Mwenyezi Mungu anasema: {Yeye ndiye wa Mwanzo (hakuna kitu kabla yake) na wa Mwisho (hakuna kitu baada yake), Aliye Juu kabisa (hakuna kitu juu yake) na Aliye Karibu zaidi (hakuna kitu kilicho karibu kuliko Yeye). Naye ni Mjuzi wa kila kitu}. (Al-Hadid, 3)
Allah says: {He is the First (nothing is before Him) and the Last (nothing is after Him), the Most High (nothing is above Him) and the Most Near (nothing is nearer than Him). And He is the All-- Knower of everything}. (Al-Hadid, 3)
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Yeye ndiye Allah ambaye hakuna mungu wa haki isipokuwa Yeye, Mjuzi wa yaliyofichika na yanayoonekana. Yeye ndiye Mwingi wa Rehema, Mwenye Huruma. Yeye ndiye Allah ambaye hakuna mungu wa haki isipokuwa Yeye, Mfalme, Mtakatifu, Aliye safi na kila kasoro, Mtoaji wa amani, Mlinzi juu ya viumbe vyake, Mwenye nguvu zote, Mwenye kulazimisha, Mwenye utukufu mkuu. Utakasifu ni wake (Yeye yuko juu) juu ya yale wanayomshirikisha nayo. Yeye ndiye Allah, Muumbaji, Mvumbuzi wa vitu vyote, Mtoaji wa maumbo. Ni wake Majina Mazuri. Kila kilichomo mbinguni na ardhini kinamtakasa Yeye. Naye ndiye Mwenye nguvu zote, Mwenye hekima}. (Al-Hashr, 22-24)
Allah the Almighty says: {He is Allah beside Whom La ilaha illa Huwa (none has the right to be worshipped but He) the AllKnower of the unseen and the seen. He is the Most Gracious, the Most Merciful. He is Allah beside Whom La ilaha illa Huwa (none has the right to be worshipped but He), the King, the Holy, the One Free from all defects, the Giver of security, the Watcher over His creatures, the All-Mighty, the Compeller, the Supreme. Glory be to Him (High is He) above all that they associate as partners with Him. He is Allah, the Creator, the Inventor of all things, the Bestower of forms. To Him belong the Best Names. All that is in the heavens and the earth glorify Him. And He is the All-Mighty, the All-Wise}. (Al-Hashr, 22-24)
(17) Kursi: kihalisi ni kiti kidogo cha miguu au kiti, na wakati mwingine hutafsiriwa kimakosa kuwa Kiti cha Enzi. Kursi inayotajwa katika aya hii inapaswa kutofautishwa na 'Arsh (Kiti cha Enzi) kilichotajwa katika Aya ya V.
(17) Kursi: literally a footstool or chair, and sometimes wrongly translated as Throne. The Kursi mentioned in this verse should be distinguished from the 'Arsh (Throne) mentioned in V.
7:58, 10:3, 85:15 na sehemu nyingine. Mtume Muhammad ﷺ alisema: "Kursi ikilinganishwa na 'Arsh si chochote isipokuwa ni kama pete iliyotupwa katika nafasi tupu ya jangwani." Ikiwa Kursi inaenea juu ya ulimwengu wote, basi 'Arsh ni kubwa zaidi kiasi gani. Hakika Allah, Muumba wa Kursi na 'Arsh wote wawili, ndiye Mkuu kabisa. Ibn Taymiyyah alisema: a) Kuamini Kursi. b) Kuamini 'Arsh (Kiti cha Enzi). Imepokewa kutoka kwa Muhammad Ibn 'Abdullah na kutoka kwa wanazuoni wengine wa dini kwamba Kursi iko mbele ya 'Arsh (Kiti cha Enzi) na iko katika kiwango cha Miguu. (Fatawa Ibn Taymiyyah, Juzuu ya 5, Kurasa 54, 55) Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (Allah amridhie): Mjumbe wa Allah ﷺ aliniamuru nilinde mapato ya Zakatul-Fitr ya Ramadhani. Kisha mtu mmoja alinijia na kuanza kuiba vyakula. Nilimkamata na kumwambia, "Nitakupeleka kwa Mjumbe wa Allah ﷺ." Kisha Abu Hurairah (Allah amridhie) alieleza simulizi yote na akasema: Yule mtu alisema (kwangu): "Tafadhali usinipeleke kwa Mjumbe wa Allah ﷺ, nami nitakufundisha maneno machache ambayo kwayo Allah atakunufaisha." Utakapoenda kulala, soma Aayatul-Kursi (2:255), kwani kutakuwa na mlinzi kutoka kwa Allah atakayekulinda usiku kucha, na Shetani hataweza kukukaribia hadi alfajiri. (Mtume ﷺ aliposikia simulizi hiyo) alisema (kwangu): "Yule aliyekujia usiku amekuambia ukweli ingawa ni mwongo; na alikuwa Shetani." (Sahih Al-Bukhari, Juzuu ya 6, Hadithi Na. 530) (Imenukuliwa na Mtafsiri)
7:58,10:3, 85:15 and elsewhere. Prophet Muhammad (Peace be upon him) said: "The Kursi compared to the `Arsh is nothing but like a ring thrown out upon open space of the desert." If the Kursi extends over the entire universe, then how much greater is the `Arsh. Indeed Allah, the Creator of both the Kursi and the `Arsh, is the Most Great. Ibn Taymiyah said. a) To believe in the Kursi. b) To believe in the 'Arsh (Throne). It is narrated from Muhammad Ibn 'Abdullah and from other religious scholars that the Kursi is in front of the `Arsh (Throne) and it is at the level of the Feet. (Fatawa Ibn Taymiyah, Vol. 5, Pages 54, 55] Narrated Abu Hurairah (May Allah be pleased with him): Allah's Messenger (Peace be upon him) ordered me to guard the Zakah revenue of Ramadan. Then somebody came to me and started stealing of the foodstuff. I caught him and said "I will take you to Allah's Messenger (Peace be upon him)." Then Abu Hurairah (May Allah be pleased with him) described the whole narration and said: That person said (to me (Please don't take me to Allah's Messenger (Peace be upon him) and I will tell you a few words by which Allah will benefit you). When you go to your bed, recite Ayat-ul-Kursi, (2:255) for then there will be a guard from Allah who will protect you all night long, and Satan will not be able to come near you till dawn. "(When the Prophet (Peace be upon him) heard the story) he said (to me), "He (who came to you at night) told you the truth although he is a liar; and it was Satan." (Sahih AlBukhari, Vol. 6, Hadith No. 530) (Quoted by Translator)