Q 206: Ni zipi bid'ah zinazohusiana na mambo ya muamala?
Q 206: What are the Innovations pertaining to dealings?
A--- Hii ni kuweka masharti ambayo hayamo katika Kitabu cha Allah (Sheria zake), wala katika Sunnah ya Nabii. Mfano ni kuweka masharti yanayoweza kubatilisha yale yaliyo halali, au kuhalalisha yale yaliyo haramu. Pia, kuweka sharti kwamba Wala' (haki ya urithi wa mtumwa aliyeachiwa huru) iwe ya mtu mwingine asiyekuwa aliyemwacha huru. Baada ya kusikia habari ya Barirah, Mtume wa Allah ﷺ alisimama mbele ya watu, na baada ya kumtukuza Allah alisema: "Amma Ba'du (yaani,
A--- This is to impose conditions which are not in neither Allah's Book (Laws), nor in the Prophetic Sunnah. Such as imposing conditions that may nullify that which is lawful, or legalize that which is unlawful. Also, stipulating the Wala,32 to be for other than the manumitter. Having heard the story of Barirah, Allah's Messenger (Peace be upon him) stood up in front of the people, and after glorifying Allah he said: "Amma Ba'du (i.e.
Halafu! Vipi kuhusu watu wanaoweka masharti ambayo hayamo katika Kitabu (Sheria) ya Allah? Sharti lolote lisilomo katika Kitabu (Sheria) ya Allah ni batili, hata kama yangekuwa mamia ya masharti, kwa kuwa hukumu za Allah ndizo za haki na masharti Yake ndiyo yenye nguvu zaidi (imara zaidi), na Wala' itakuwa ya mwenye kumwacha huru.” (Bukhari na Muslim)
then after)! What about the people who impose conditions which are not in Allah's Book (Laws)? Any condition that is not in Allah's Book (Laws) is invalid even if they were one hundred conditions, for Allah's decisions are the right ones and His conditions are the strong ones (firmer) and the Wala' will be for the manumitter.”(Bukhari and Muslim)
Marejeo: 200 FAQ On Muslims Belief - Shiekh Hafiz Ibn Ahmed Al Hakami
Reference: 200 FAQ On Muslims Belief - Shiekh Hafiz Ibn Ahmed Al Hakami