Q 21: Ni dalili gani za kimaandiko kutoka katika Qur'ani Tukufu na Sunnah ya Mtume (Hadithi) kwamba Muislamu lazima awe na imani kamili?
Q 21: What is the textual proof from the Glorious Qur'an and the Prophetic Sunnah (Tradition) that a Muslim must have absolute faith?
A--- Allah Mtukufu asema: {Hakika waumini ni wale tu waliomwamini Allah na Mtume Wake, kisha wasitilie shaka, na wakapigania kwa mali zao na nafsi zao katika Njia ya Allah.
A--- Allah the Almighty says: {Only those are the believers who have believed in Allah and His Messenger, and afterward doubt not but strive with their wealth and their lives for the Cause of Allah.
Hao ndio wakweli.}
Those! They are the truthful}. (Al-Hujurat, 15)
Nabii Muhammad ﷺ anasema: "Ninashuhudia kwamba hakuna mungu isipokuwa Allah, na mimi ni Mtume Wake. Mja yeyote atakayekutana na Allah bila ya kuwa na shaka yoyote kuhusu (misingi hii miwili), ataingia peponi." (Muslim)
Prophet Muhammad (Peace be upon him) says: "I bear testimony to the fact that there is no god but Allah, and I am His messenger. The slave who would meet Allah without entertaining any doubt about these (two fundamentals) would enter heaven ". (Muslim)
Mtume Muhammad ﷺ alimwambia Abu Hurairah (Allah amridhie): "Chukua viatu hivi vyangu, na utakapokutana na yeyote nje ya bustani hii anayeshuhudia kwamba hakuna mungu isipokuwa Allah, akiwa na uhakika nayo moyoni mwake, mfurahishe kwa kumtangazia kwamba ataingia Peponi." (Sahih Muslim)
Prophet Muhammad (Peace be upon him) said to Abu Hurairah (May Allah be pleased with him): "Take these sandals of mine, and when you meet anyone outside this garden who testifies that there is no god but Allah, being assured of it in his heart, gladden him by announcing that he shall go to Paradise ". (Sahih Muslim)
Marejeo: 200 FAQ On Muslims Belief - Shiekh Hafiz Ibn Ahmed Al Hakami
Reference: 200 FAQ On Muslims Belief - Shiekh Hafiz Ibn Ahmed Al Hakami